Halaal

________________________________________________________________________________

UTANGULIZI

Kunzishwa kwa Mamlaka ya Halal Tanzania kunatokana na hitajio kubwa la kuwapo kwa udhibiti wa vyakula na vinywaji halal kwa mujibu wa Sheria na Shariah ambapo kwa mazingira ya sasa,  ni jambo linalohitajika sana kwa ajili ya Afya ya Mlaji na Ustawi wa Jamii kwa Ujumla.

________________________________________________________________________________

HALAL BUREAU – TANZANIA

Halal Bureau – Tanzania ni Taasisi ya Kijamii iliyoundwa na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania (BARAZA KUU) kwa kushirikiana na Watendaji – Wataalamu toka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zikiwemo: TAMPRO, HAIATUL ULAMAA na BASUTA. Imesajiliwa BRELA, Oktoba 02, 2012 na kupewa Namba ya Usajili 93244 kwa jina la Halal Bureau Ltd kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni 2002 (kwa Udhamini bila Hisa) kwa ajili ya kuihudumia Jamii.

MAKAO MAKUU

Makao Makuu ya Halal Bureau yapo Kinondoni ‘B’, Barabara ya Kawawa/Isere MNY/314 A ambapo pamoja na majukumu mengine; ndiyo Ofisi inayoratibu kazi na majukumu ya matawi yake yote nchini ikisaidiwa na Ofisi za Kanda zilizopo katika mikoa ya: Dar es Salaam, Tabora, Tanga (Arusha), Mtwara, Iringa (Mbeya),  Mwanza, Dodoma na Mji Mkongwe Unguja.

DIRA

Dira ya Halal Bureau Tanzania ni “Utambuzi wa Halal ni Haki ya Watu Wote kwa Ustawi na Maendeleo ya Taifa”.

DHAMIRA

Dhamira ya Halal Bureau ni “Kuraghibisha Jamii kupata ithibati kuhusu Halal katika vyakula, vinywaji na bidhaa zingine zitumikazo bila ya kujali rangi, kabila au dini ya Mtumiaji, Mzalishaji na au Muuzaji”.

LENGO

Ni Umma kuwa na utambuzi na kujua nafasi yake katika kusaidia kushajiisha matumizi mazuri ya dhana ya Halal bila mtengano kwa maslahi yaTaifa.

MADHUMUNI

Ili kufanikisha Dira, Dhamira na Lengo, Halal Bureau inasimamia Madhumuni yafuatayo:

Kuraghibisha Umma kuwa makini katika matumizi ya Halal

Kuujuza Umma kuhusu Taarifa za Halal: Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kuujengea Umma kuishi kwa uadilifu miongoni mwa wanajamii.

Kutoa Elimu ya Utambuzi wa Halal: ili kuepuka mikanganyiko hususani inayoweza kufanywa na watu wasiokuwa waadilifu.

Kudhibiti Ubora wa Bidhaa Halal: Kwa lengo la kumpa haki Mlaji kutolishwa bidhaa isiyohusika.

Kuhimiza Umma kutumia Bidhaa zenye utambulisho wa halal bila KULAZIMISHWA.

Kushirikiana na wadau wengine katika kulinda Afya ya Mlaji kwa kulinda Ubora wa Bidhaa, Vipimo, Kanuni za Utunzaji wa Mazingira na Nidhamu ya Kudhibiti Mateso kwa Wanyama.

SHUGHULI ZINAZOFANYWA

Ukaguzi (Inspection): Hufanywa kabla kwa wanaoomba na pia wakati wowote kwa wale waliokwishathibitishwa kuwa na bidhaa na au kutoa huduma zilizo Halal kwa ajili ya Uhakiki.

Uchambuzi/Uchunguzi (Analysis): Kubainisha Vijenzi (ingredients) ambavyo ni Mush’bohaat (Vyenye Utata) hususani kwa bidhaa iliyoombewa na Mmiliki husika kuthibitishwa uhalali wake.

Usimamizi (Supervision): Usimamizi huu hufanywa kwa lengo la kudhibiti utaratibu wa kuhakiki halal hususani kwa shughuli zinazojitegemea na ambazo uzalishaji wake hufanyika kila siku: Machinjioni, Migahawani, n.k.

Usimamizi wa Usafi (Hygiene): Ni kuratibu na kusimamia uzingativu wa Usafi katika maeneo ya Uzalishaji, Utunzaji Usafirishaji na Udhibiti wake dhidi ya Mazingira Machafu na au Bidhaa zisizo halal.

Uhakiki (Auditing): Ili kudhibiti uhalifu kwa jina la Halal, Ukaguzi huu unaofanywa kwa lengo la kuhakiki Maeneo, Huduma, na au Bidhaa iliyokwishathibitishwa kuwa ni halal, ikibainika kuwapo kwa ukiukaji wa taratibu, hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mhusika kwa mujibu wa mkataba uliowekwa kwa maslahi ya Jamii na Afya ya Mlaji.

Uthibitishaji (Accreditation): Cheti/Leseni hutolewa kwa Huduma na au bidhaa husika iwapo imekidhi vigezo vya Halal. Pamoja na ithibati hiyo pia hupata ruhusa kutumia nembo ya HALAL BUREAU kwenye Bidhaa na au huduma husika kwa masharti ya Halal.

Ushauri (Consultancy): Huduma hii ya Ushauri hutolewa kwa Bidhaa au huduma husika kwa lengo la kumakinisha uhalal wake na au kuifanya ifikie vigezo vya kuthibitishwa kuwa na viwango vya kuwa ni halal

Utoaji wa Mafunzo Kwa Wadau Kuhusu Halal: Mafunzo hayo yanawahusu watu wa kada mbalimbali bila kujali dini wala makabila yao: Miongoni mwa kada hizo ni Wasomi wa fani za Vyakula, Kemikali, Madaktari, Wanasheria, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kijamii, Kisiasa n.k.

MAWASILIANO:

Kwa Maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kwa anuani zifuatazo:

1)     MAKAO MAKUU

S.L.P 10993 Dar es Salaam

SIMU 0784 953 981 / 0754 362264

BARUA PEPE: halal@barazakuutanzania.org

Kinondoni B, Barabara ya Kawawa na Mtaa wa Isere, Nyumba MNY/314 A

2)     Kanda ya Ziwa Magharibi – Tabora – Kigoma na Katavi

S.L.P. 1709 Tabora

SIMU:  +255 759 080626

BARUA PEPE: halal@barazakuutanzania.org

Kata ya Kanyenye, Mtaa wa Madrasa, Tabora Mjini.

3)     Kanda ya Kaskazini – Tanga / Arusha – Kilimanjaro na Manyara

S.L.P. 6219 Arusha

SIMU +255 765 824 521

BARUA PEPE: halal@barazakuutanzania.org

Mtaa wa Bondeni, Mkabala na Msikiti Mkuu wa Ijumaa Bondeni

4)     Kanda ya Kusini – Mtwara – Mtwara na Lindi

S.L.P. 1353 Mtwara

SIMU +255 232 334 546

BARUA PEPE: halal@barazakuutanzania.org

Mtaa wa Muungano Mkabala na Mahakama ya Mwanzo, Plot No 582

5)     Nyanda za Juu Kusini – Iringa /Mbeya – Ruvuma, Njombe na Rukwa

S.L.P. Mbeya

SIMU 0784 953 981 / 0754 362264

BARUA PEPE: halal@barazakuutanzania.org

Kinondoni B, Barabara ya Kawawa na Mtaa wa Isere, Nyumba MNY/314 A

6)     Kanda ya Ziwa- Mwanza – Mara, Kagera, Geita, Shinyanga na Simiyu

S.L.P. 5253 Mwanza

SIMU: +255 737 202 684, + 255762 077 184

BARUA PEPE: halal@barazakuutanzania.org

Kata ya Mirongo, Mtaa wa Mtakuja, Nyamagana, Plot 70 Block MZ/295

7)     Kanda ya Kati – Dodoma – Dodoma na Singida

S.L.P. 2143 Dodoma

SIMU +255 262 320 300,  +255 715632732

BARUA PEPE: halal@barazakuutanzania.org

Kata ya Majengo, Kariakoo Bazaar, Soko la Matunda. 

8)     Kanda ya Visiwani – Mji Mkogwe – Unguja na Pemba

SLP 10993 Zanzibar

SIMU +255 766 295 353, +255 773 985 858

BARUA PEPE: halal@barazakuutanzania.org

Malindi, Mji Mkongwe Darajani – Unguja.